SEKRETARIETI MPYA CCM KUTANGAZWA LEO

 Chama Cha Mapinduzi on Twitter: "Wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu  ya Taifa ya CCM wakijadiliana jambo kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu  kilichoketi leo tarehe 9 Julai 2020

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Philip Mangula amesema baada ya kumchagua Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Samia Suluhu Hassan, kazi itaendelea ili kuiteua na kuitangaza Sekretarieti mpya.

Moja ya nafasi inayosubiriwa kwa hamu kubwa ni ile ya Katibu Mkuu wa chama hicho ambayo imekuwa wazi tangu Bashiru Ally Kakurwa alipoteuliwa na baadaye kuondolewa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi.

"Zege halilali," alisema Mwenyekiti Mpya Mama Samia wakati akiufunga rasmi mkutano mkuu maalum, huku akiwataka wajumbe wa Halmashauri Kuu kuendelea kusubiri ili kuimaliza kazi hiyo leo hii hii.

No comments