PRESHA WAKUU WA MIKOA, WILAYA, MADED

 

BAADA ya Rais Samia Suluhu Hassan kufanya marekebisho kadhaa katika nafasi za Mawaziri, Manaibu Mawaziri, Katibu Mkuu Kiongozi, Makatibu Wakuu wa Wizara, Manaibu  Makatibu Wakuu na Taasisi za Serikali, sasa yu mbioni kufanya hivyo kwa Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri.

Presha kwa viongozi hao wa kisiasa imepanda, kwani hakuna mwenye uhakika wa kubakia kwenye nafasi yake, achilia mbali kubadilishwa kutoka sehemu moja hadi nyingine.

Wakatgi wa uongozi wake, Rais wa Awamu ya Tano, John Joseph Pombe Magufuli, aliwapa nafasi hizo baadhi ya watu walioonekana kama wenye kujipendekeza, kumsifu kupita kiasi na ambao sifa yao kubwa ilikuwa ni kuwanyanyasa wapinzani wa CCM.

Baadhi ya wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi wamekuwa wakilaumiwa na wananchi wa maeneo yao, wakionekana kutofanya kazi zao sawasawa, hivyo kutamani mabadiliko kutoka kwa Mama Samia maarufu kama Sasha.

 

 

No comments