NI UTOTO, SEMA TATIZO WANA HELA

YES, kwa vigezo
vyovyote, hawa wasanii wawili, Konde Boy na Ran Vany, ni watoto. Sio kiumri
pekee, lakini hata kimuziki.
Katika umri, ni
daraja moja na watoto weeeengi waliopo Bongo Fleva hivi sasa, ambao nyakati
zinawabeba kwa sababu ya mitandao ya kijamii na tofauti na kaka zao, wana
hawana bughudha yoyote kutoka kwa Wahindi.
Sina uhakika
ninaposema wahindi kama wananielewa hawa watoto. Wasanii wa siku hizi wanapata
hela hata kama wasipopata nafasi ya kupanda jukwaani.
Kaka zao
iliwalazimu kutengeneza albamu kama watataka kupata hela na zaidi, hawakuwa na
uwezo wa kuidhibiti albamu hiyo sokoni. Na ndiyo maana kuna watu
walijitengenezea 'ufalme' wa sanaa ya muziki japo hawakuwa wanamuziki. Kama
hupati nafasi ya kuperfom jukwaani, utapataje hela?
Wameikuta sanaa
katika mteremko, kiasi kwamba kwao imekuwa rahisi mno kutoka. Wakongwe waliopo
katika muziki, sidhani kama wanayo furaha wakiona jinsi hawa watoto wanavyopiga
hela kirahisi wakati wenyewe walihenya kwelikweli.
Leo hii, Profesa
Jay anakwenda kufanya mahojiano katika redio na televisheni inayomilikiwa na
Diamond Platnumz, mtoto ambaye wakati Jay akiwa katika zama zake, alitamani
hata kushika tu pale aliposhika ili kuipa furaha nafsi yake.
Kama muziki
ungetenda haki bila kujali nyakati, leo hii Sugu angekuwa anamiliki kiwanda
kikubwa tu cha kutengeneza vinywaji vikali vinavyouzwa zaidi katika Ukanda wa
Afrika Mashariki na Kati.
Lady Jaydee leo
hii, pengine angekuwa ndiye mkulima mkubwa zaidi wa nafaka kwa nchi za Sadc,
hivyo kuingiza mamilioni ya shilingi akiwa na ofisi katika nchi zote hizo.
Wachache waliofanya
vizuri wakati huo, walifanya hivyo pasi na kuwa na kile leo wanachokiita
menejimenti, maana wengi wa namna hiyo walikuwa ni wanyonyaji.
Na bifu hazijaanza
leo, zilianza zamani tu ndani ya Bongo Fleva. Ingawa nyingi ya bifu za zamani
zilitengenezwa ili kuwanyoosha walioenda kinyume na walioushika muziki, lakini
zilikuwepo.
Watu walishindana
kwanza kwa kuandika mistari mikali na yenye funzo ndani yake, ndipo zinakuja tambo.
Hawakufikia hatua
hii ya hawa watoto wawili kuanza kuanikana na kujipa aibu inayozuilika. Licha
ya utoto wao, lakini kinachowapa jeuri ya kuuleta utoto wao mbele ya watu
wazima, ni uwezo wao wa kifedha pia.
Watoto wana hela. Wanaweza,
bila wasiwasi wowote, kusafiri na kwenda kutanua popote duniani. Unapopata
uwezo huu, halafu ukiwa bado mtoto, ni mara chache busara inakuwa upande wako.
Wangekuwa na akili
baada ya kupata hizo fedha zao, wala tusingesikia ujinga huu unaoendelea. Baada
ya Konde Boy kutoka pale Wasafi, kama watoto wote walivyo, anaamini lebo kama
lebo haijapenda na hivyo itamfanyia mizengwe mingi kumkwamisha.
Ukisikiliza nyimbo
za Konde Boy baada ya kutoka Wasafi, utabaini hiki ninachokisema. Ana madongo
flani hivi ya waziwazi na mlengwa wa hizo jumbe ni Diamond.
Bahati nzuri,
Diamond ni next level. Anajua yeye kama yeye hadhi yake kimuziki ni kubwa
kuliko Konde Boy, so ili kutompa mileage, hajibishani naye. Kazi hiyo inafanywa
na menejimenti yake.
Harmonize
analazimisha jamii ione WCB ni wabaya wake. Kama kuondoka kwenye chama lao ni
sababu ya chuki, mbona hatusikii hayo mambo yakifanywa kwa Rich Mavoko, ambaye
mimi binafsi naamini Mavoko ni msanii mkubwa kuliko Harmo?
Baada ya kuona
Diamond hajibishani naye, akageukia kwa wasanii wa levo yake. Nani haelewi
jinsi Konde Boy alivyokuja juu, baada ya Ran Vanny kuleta utoto wake kwa
kuvujisha video akiwa na yule mtoto mwenzie kimahaba?
Na utoto wao
ulianzia hapo. Hakukuwa na sababu yoyote kwa Ran Vanny kuwaambia watu kuwa
anatoka na yule mtoto mwenzie. Ninafahamu kuna wasanii wenzake walijua, akiwemo
Harmonize, lakini hawakuwa na ushahidi.
Kitendo chake cha
kuvujisha ile video kiliwapa watu nafasi ya kuongea. Mimi nitakuwa wa mwisho
kuamini kuwa Kajala hakuwa akijua kama mtoto wake yupo na huyu dogo wa WCB.
Kitendo cha kusema sijui Mobeto ndiye aliyempeleka huko lanchi, ni kutafuta
huruma tu kwa jamii na vile yeye ni mama lazima awe na kitu cha kuongea.
Harmonize hakupaswa
kuja juu namna ile alivyokuja. Mbona kwa wasanii ni jambo dogo na la kawaida tutu?
Anaweza kusimama na kuapa mbele ya mola kwamba yeye hajawahi kutoka na under
17? Nitakuwa wa mwisho kulikubali hili!
Paniki yake na nia
yake ya kutaka vyombo vya sheria vifanye kazi yake, ilithibitisha chuki yake
kwa WCB, na ndiyo maana menejimenti ilikuja juu sana kumpinga kwenye hii ishu.
Walijua dogo anataka kuharibu image ya lebo yao.
Utoto mwingine ni
wa Harmonize mwenyewe. Unapigaje picha za utupu na kumtumia mpenzi au mwanamke
unayetamani awe mpenzi wako? Well, inawezekana pengine hakutuma picha za utupu
wake au wa mtu mwingine, lakini meseji iliyo wazi hapa ni kuwa Harmonize
alikuwa na mawasiliano ya kimapenzi na kile kitoto cha Kajala!
Na upo ushahidi wa
kimazingira kuwa meseji hizo alikuwa anapewa RanVanny. Bahati mbaya, kwa utoto
wake, alishindwa kutuliza kichwa chake kufanya kazi sawasawa. Angeweza
kuvujisha picha hizi bila kutumia akaunti yake.
Lakini aliamua
kutumia akaunti yake kwa sababu tu alitaka Harmonize ajue kuwa yeye ni nani! Ni
utoto tu unaowafanya hawa watoto wafikie hatua hiyo.
Unashangaa ni vipi
Baba Levo, Diwani mstaafu naye aliweza kuingizwa kwenye utoto huu na hawa
watoto.
Haya yote
yanafanyika kwa sababu ya kuwa wana fedha. Wanajua mwisho wa siku watapelekana
mahakamani na kutakiwa kulipa faini. Watalipa.
Wasichojua ni kwamba
sheria ina kawaida ya kutotulia. Kosa na hukumu ya jana, siyo itakayohukumu
kosa lilelile likifanyika kesho.
Ndiyo maana wasanii
wengi huko mbele wanafungwa jela kwa sababu wanajua wanao uwezo wa kulipa
faini, hivyo njia pekee ya kuwafanya waheshimu sheria ni jela.

Post a Comment