MSIKIE RYAN GIGGS AKIMZUNGUMZIA KAKA!!!

KAMA kuna mchezaji ambaye ninahisi kumpenda ndani ya moyo wangu kwa
uwezo wake uwanjani, uungwana wake, hadhi yake na ubinadamu, bila shaka yoyote
atakuwa ni Ricardo Kaka.
Tulikutana katika nusu fainali
ya Ligi ya Mabingwa pale Old Trafford na Kaka alikuwa hakabiki, alikuwa na
kiwango ambacho kilikuwa cha juu mno katika yale mashindano ambacho kilileta
tofauti. Ilikuwa ni mara yetu ya kwanza kukutana uwanjani.
Kuna wakati katikati ya uwanja nilimchezea
faulo, akanisogelea na kunikaba shingoni na yeye alipewa kadi kwa kitendo
hicho. Nilijua wakati huo kuwa alikuwa ni mtu wa dini na ameokoka, lakini
nikajiuliza, mtu wa imani kiasi hicho anawezaje kunikaba hivi?
Mchezo ulipoisha tukiingia
katika vyumba vyetu vya kubadilishia nguo, alikuwa akinisubiri akiwa na Gennaro
Gattuso ambaye alikuwa akiongea Kiingereza vizuri kwa sababu aliwahi kuichezea Rangers.
Gattuso aliniambia kuwa Ricardo alitaka
kuniomba radhi kwa kitendo chake kisicho cha kiungwana alichonifanyia. Nikasema
haina taabu, sisi wote ni binadamu.
Ricardo alinikumbatia na
akanipatia msalaba. Nilishtuka sana kwa uungwana wake na nikamwambia "Ricardo,
usijali, wachezaji wakiwa uwanjani wakati mwingine hufanya mambo ya ajabu sana,
lakini katika Ligi ya Mabingwa na hasa katika mchezo wa Nusu Fainali, hivi ni
vitu vya kawaida.
Gattuso alifanya vizuri sana
katika kutafsiri na Kaka akapiga magoti mbele yangu na akanishukuru tena.
Wachezaji wote ndani ya chumba cha kubalishia nguo walishangilia na
tukabadilishana jezi. Zawadi yake bado ninayo na inanikumbusha moja kati ya
matukio muhimu zaidi katika maisha yangu ya soka.

Post a Comment