MAMA JANETI MAGUFULI MGONJWA

Kwa mujibu wa mtoto wa marehemu John Joseph Magufuli, aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Tanzania, Janeti Magufuli, ambaye ni mkewe, ni mgonjwa.
Joseph Magufuli, ambaye alitoa salamu za familia ya marehemu kwenye kongamano la kidini jana, alisema mama yake, Janeti hajisikii vizuri kutokana na mshtuko wa kifo cha mumewe, kilichotangazwa Machi 17, mwaka huu.
Alisema mama yake angeweza kufika katika tukio hilo, lakini hali yake kiafya hairuhusu. Hata hivyo, mtoto huyo alitoa salamu za mama yake, akisema anawasalimu na kuwashukuru watanzania wote na kwamba anawapenda sana.

Post a Comment