MADAM SAMIA SULUHU HASSAN MWENYEKITI CCM

RAIS wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan maarufu kama Sasha, leo atapewa
nafasi ya Uenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, mbele ya Mkutano Mkuu Maalum wa
chama hicho kikongwe.
Hii inafuatia kifo
cha Mwenyekiti aliyetangulia, John Pombe Magufuli, ambaye alifariki dunia Machi
17 mwaka huu kwa ugonjwa wa moyo katika Hospitali ya Mzena, Kinondoni jijini
Dar es Salaam.
Maandalizi yote ya
mkutano huo yamekamilika na wajumbe wote wameshawasili jijini Dodoma, tayari
kwa mkutano huo utakaofanyika katika ukumbi wa chama hicho.
Wakati Mama Samia
akikabidhiwa nafasi hiyo ya juu kabisa katika chama hicho, Makamu wa Mwenyekiti
wa CCM Zanzibar, Dk. Mohamed Shein, naye anatarajiwa kumkabidhi wadhifa huo
Rais wa sasa wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi.

Post a Comment