KAGERE, DUBE WACHUANA KILELENI

 www.kigalitoday.com/IMG/jpg/kagere_meddie-2.jpg

Prince Dube, mshambuliaji nyota wa Azam, amefikisha mabao 11 katika Ligi Kuu Tanzania Bara, sasa akiwa anapambana na washambuliaji wa Simba Meddie Kagere mwenye idadi kama hiyo ya mabao na John Bocco ambaye ameingia kambani mara kumi.

Washambuliaji wengi wameshindwa kupambana na Kagere tangu ameingia nchini kwa sababu misimu yote aliyocheza VPL amekuwa mfungaji bora.

Mazingira ya Dube na Kagere msimu huu yanafanana kwa kiasi fulani, wote wamekosa baadhi ya mechi za ligi, Dube alipata majeraha na akakaa kwa muda nje ya uwanja lakini Kagere anaathiriwa na makocha wa timu yake kufanya rotation kwenye eneo la ufungaji.

Kagere amekuwa hana uhakika wa kucheza mfululizo kama ilivyokuwa misimu miwili iliyopita lakini hawa watu [Dube na Kagere] wanatuonesha kuwa, kazi ya kufunga wanaweza kuifanya kwa ufasaha ndio maana pamoja na kucheza mechi chache bado wanashindana kwenye orodha ya wafungaji.


No comments