MWILI WA JPM WAWASILI ZANZIBAR
MWILI wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Joseph Magufuli umewasili Zanzibar asubuhi hii na kupokewa na Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi, sambamba na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Ukiwa umebebwa na maofisa wa ngazi za juu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, mwili huo ulishushwa katika ndege na kupelekwa na kupakiwa katika gari maalum la wazi, kabla ya safari ya kuanza kuelekea Uwanja wa Amaan, ambako mamia ya wananchi watauaga.
Katika barabara kadhaa ambako mwili huo ulipita, maelfu ya wananchi walikuwa wamejipanga huku wakipunga mikono, majani na kutandika kanga, kuonyesha mapenzi yao kwa rais huyo wa kwanza nchini kufariki akiwa madarakani.

Post a Comment