KENYATTA, NYUSI KAMA WASWAHILI TU!


 RAIS Uhuru Kenyatta wa Kenya na mwenzake wa Msumbiji, Filipe Nyusi, leo walikuwa ni kama waswahili tu baada ya kutoa hotuba zao kwa Kiswahili fasaha na kushangiliwa sana na mamia ya waombolezaji waliofurika katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma wakati wa kumuaga Rais John Pombe Magufuli anayezikwa Ijumaa hii.

Wawili hao walikuwa ni miongoni mwa marais na wawakilishi wa serikali zaidi ya 17, waliokuwepo kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho mwa JPM, mbaye alifariki dunia Machi 17 mwaka huu kwa maradhi ya moyo.

 

No comments