MSIKIE JOSE MOURINHO KWA MARIO BALOTELI

Ex Liverpool Star Mario Balotelli Signs For Silvio Berlusconi's AC Monza

  

NINGEWEZA kuandika kitabu cha kurasa 200 katika miaka yangu miwili nikiwa na        Inter Milan na Mario, lakini kitabu hicho kisingekuwa cha maana, kingekuwa ni vichekesho.

 

Nakumbuka kuna wakati mmoja tulienda kucheza na Kazan katika Ligi ya Mabingwa. Katika mechi ile washambuliaji wangu wote walikuwa majeruhi, hakukuwa na Diego Milito wala Samuel Eto’o, hakika nilikuwa katika kikaango na mtu pekee niliyekuwa naye alikuwa ni Mario.

 

Mario alipewa kadi ya njano katika dakika ya 42, kwa hiyo wakati wa mapumziko nilitumia dakika 14 kati ya 15 kuzungumza naye.

“Nilimwambia, Mario, siwezi kukutoa, sina mshambuliaji katika benchi, kwa hiyo usimguse mtu, wewe cheza mpira tu, ukinyang'anywa mpira tulia, mtu akikupa presha, wewe mpuuze, refa akikosea, wewe uchune,

Dakika moja tu baada ya mpira kuanza, kadi nyekundu!

 

 

No comments