Tanapa yatangaza Utalii Ulaya Kaskazini -- "My Tanzania roadshow 2024'
Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limeshiriki katika msafara wa kutangaza utalii nchi za Ulaya Kaskazini ambazo ni Berlin-Germany, Copenhagen -Denmark, Oslo-Norway na Stockholm-Sweden yaliyoanza tarehe 29.4. hadi 3.5.2024. Msafara huu wa utalii unaojulikana kama "My Tanzania Roadshow" umeratibiwa na kampuni ya KILIFAIR kutoka Tanzania.
Aidha katika msafara huu jumla ya makampuni ya utalii 20 kutoka Tanzania yameshiriki wakiwemo mawakala wa usafirishaji, huduma za malazi pamoja na waendesha utalii wa puto.
"My Tanzania Roadshow 2024" imetoa fursa kwa ujumbe kutoka Tanzania kukutana na “Travel Agencies” zaidi ya 120 kutoka Germany, Denmark, Norway na Sweden.
Huu ni muendelezo wa kutangaza utalii na kuvutia uwekezaji katika masoko mapya yalioonesha ukuaji wa kasi katika kipindi kifupi pamoja na kuendelea kuhamasisha kwenye masoko ya zamani ili kufikia malengo ya kitaifa Tanzania kufikisha wageni milioni tano na mapato ya dola za kimarekani bilioni sita ifikapo mwaka 2025.

Post a Comment