Wanajeshi wanne wa Israel wajeruhiwa katika mlipuko wa Hezbollah - IDF
Kwingineko katika Mashariki ya Kati, Israel inasema wanajeshi wake wanne wamejeruhiwa, mmoja vibaya sana, katika mlipuko uliotokea usiku kucha katika "eneo la mpakani" kaskazini mwa Lebanon.
Kundi la Hezbollah la Lebanon, ambalo mara kwa mara limekuwa likipambana na wanajeshi wa Israel kaskazini, linasema kuwa vikosi vyake vililipua vilipuzi baada ya wanajeshi wa Israel kuvuka mpaka katika ardhi ya Lebanon.
Jeshi la Israel halikuthibitisha iwapo vikosi vyake viliingia Lebanon.
Hezbollah ni kundi la wanamgambo wa Kishia wa Lebanon wenye uhusiano wa karibu na Iran na mshirika wa Hamas. Imekuwa ikifanya mapigano ya kuvuka mpaka na Israel karibu kila siku tangu vita vilipozuka kati ya Israel na Hamas.
BBC

Post a Comment