Step by Step ya Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Pwani yaendelea Tarafa ya Ruvu leo
Ziara ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Pwani, David Mramba katika Wilaya ya Kibaha Vijijini inaendelea na leo itakua katika tarafa ya Ruvu yenye Kata nne.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ofisi yake, ilisema leo atafanya ziara katika Kata za Kwala, Dutumi, Kikongo na Ruvu kuanzia saa nne asubuhi hadi saa kumi jioni.
Lengo la ziara hiyo ni kutoa mafunzo ya Itikadi na Ujenzi wa chama katika wilaya hiyo, kutekeleza adhima ya kuufanya mkoa huo mkubwa kieneo katika ukanda wa pwani ya Bahari ya Hindi kuwa wa kijani.

Post a Comment