RC ROSEMARY SENYAMULE AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI NOLUTHANDO MAYENDE WA AFRIKA KUSINI NCHINI JIJINI DODOMA
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule wiki hii Aprili 12, 2024 amempokea Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania Mhe. Noluthando Mayende akiwa na ujumbe wake na kufanya mazungumzo katika ofisi yake iliyopo jengo la Mkapa Jijini Dodoma.
Lengo la ujio huo ni kufanya mazungumzo yatakayowezesha ushirikiano kati ya Mkoa wa Dodoma na nchi ya Afrika Kusini.
Mhe. Balozi aliambatana na Bi. Ndumiso Mngadi Afisa wa Ubalozi, Bw. Msaneza Bilonkwa, Katibu wa Kijamii na Bw. Emmanuel Shayo, Afisa Mwandamizi wa Mambo ya Nje.

Post a Comment