MWENYEKITI WA CCM MKOA WA RUVUMA ASISITIZA UMOJA NA MSHIKAMANO KWA WANACCM WILAYA YA MBINGA

 


Chama Cha Mapinduzi CCM mkoa wa Ruvuma kupitia Mwenyekiti wake  comrade Oddo Kilian Mwisho jana April 14 -2024 Ameiongoza kamati ya siasa Mkoa kufanya ziara wilayani Mbinga katika Kata ya Utiri iliyopo Halmashauri ya Mbinga Mji.

Akizungumza katika vikao viwili tofauti yaani kikao cha waheshimiwa Madiwani wa CCM kutoka  Halmashauri ya Mbinga mji  na viongozi  wa chama Cha mapinduzi ngazi ya mashina, matawi, na Kata ya Utiri , Mwenyekiti Oddo Mwisho amewashukuru na kuwapongeza Kwa ushindi wa uchaguzi mdogo wa Kata hiyo hasa Kwa kuichagua CCM na mgombea wake Ndugu. Herswida Komba kuwa diwani wa Kata hiyo, (ikumbukwe uchaguzi huo mdogo  uliofanyika Machi 20-2024)

Mwenyekiti Oddo ameongeza kwa kusema, wanachama wote wa Kata ya Utiri, wilaya ya Mbinga, na Mkoa wa Ruvuma Kwa ujumla, kuwa na Upendo, umoja na mshikamano Ili kuimarisha ngome ya ushindi kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 na uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 na kuhakikisha CCM inashinda Kwa kishindo, kuanzia vitongoji,vijiji, mitaa, udiwani, ubunge na Urais.

Naye Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mbinga Ndugu Joseph Mdaka akishukuru Kwa niaba ya WANACCM wilaya, Amempongeza mwenyekiti huyo na  kamati nzima ya siasa Mkoa Kwa usimamizi na uongozi Bora uliotukuka, Nakuahidi kuendelea kudumisha  umoja na mshikamano Kwa wanachama wote wa CCM na jumuiya zake wilayani Mbinga,


Imetolewa na Idara ya itikadi Uenezi na Mafunzo ya chama Cha mapinduzi CCM wilaya ya Mbinga.

No comments