Mwenezi Pwani aanza ziara Step by Step Tarafa ya Mlandizi kutoa mafunzo ya Itifaki na Ujenzi wa Chama


Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo CCM Mkoa wa Pwani *Ndg. David Mramba* ameianza ziara yake aliyoipa jina la *STEP BY STEP* katika Tarafa ya Mlandizi, Wilaya ya Kibaha vijijini Leo *Tarehe 24, April 2024* katika Ukumbi wa Pentagon uliopo karibu na Stendi ya magari.

Katika Ziara hiyo, *Ndg. David Mramba* ametoa Mafunzo mbalimbali kwa Makatibu wa CCM na Wenezi wa Matawi, Makatibu wa CCM na Wenezi wa Kata za Tarafa hiyo na Makatibu wa Hamasa wa Kata hizo yakiwemo Mafunzo ya Itifaki ya ukaaji, Itifaki ya bendera, Itifaki ya Magari na Itifaki ya Mavazi, Uongozi na Maadili.

Pia, *Ndg. Mramba* ameendelea kuwasisitiza wanachama kuendelea kuheshimiana, kuthaminiana, na kusaidiana ili kufikia malengo ya Chama.

Amesema ni wajibu wa Kila mwanachama kulipa ada na kujitoa ndani ya Chama huku akiwataka kutimiza majukumu yao kutokana na Katiba ya CCM inavyoeleza.

Aidha, amewataka wanachama wa CCM Kibaha Vijijini kuwa wamoja ili kukijenga chama na kujiandaa madhubuti na Chaguzi zilizo mbele yao *2024*  Chaguzi za Serikali za Mitaa, Vijiji, Vitongoji, na *2025* uchaguzi Mkuu.

Amewakumbusha kuwa nafasi walizo nazo ni dhamana hivyo wanatakiwa kuzitumia kwa maslahi ya Chama na si kwa maslahi Yao binafsi.

Mwisho, amewakemea baadhi ya wanachama kuanza kuandaa wagombea kabla ya muda wa uchaguzi jambo ambalo linatengeneza Makundi na kukigawa chama.


 Step By Step

# 2024 Pwani ya Kijani

 Samia Mitano tena


 Imetolewa na: Idara ya Siasa, Uenezi na Mafunzo CCM,

Mkoa wa Pwani


KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

No comments