MKURUGENZI MANISPAA YA TEMEKE AIPONGEZA TARURA KURUDISHA MAWASILIANO YA BARABARA
Temeke
Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Elihuruma Mabelya ameipongeza Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kwa kurudisha mawasiliano ya barabara katika Manispaa yake zilizoharibika kutokana na mvua.
Mabelya ameyasema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Meneja wa TARURA mkoa wa Dar es Salaam Mhandisi Geofrey Mkinga pamoja na timu ya wataalamu wa Mazingira na Ustawi wa Jamii kutoka TARURA Makao Makuu kwenye ofisi za Manispaa hiyo jijini Dar es Salaam.
Katika mazungumzo yao walijadiliana kuendelea kuboresha mkakati wa Usafi na utunzwaji wa mitaro pamoja na miundombinu ya barabara wilayani hapo.
Timu ya wataalamu kutoka Kitengo cha Mazingira na Ustawi TARURA inaendelea kufanya mazungumzo na Wakuu wa Wilaya kwa lengo la kufanya uhamasishaji kuhusu usimamizi wa sheria ya mazingira zilizo chini ya mamlaka ya Manispaa na Jiji katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Post a Comment