KATIBU MKUU CCM ALIVYOPOKELEWA KICHIFU SONGEA
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Emmanuel Nchimbi amekaribishwa rasmi nyumbani kwao Mkoa wa Ruvuma kwa kufanyiwa kimila na machifu pamoja na wazee wa jadi alipofika eneo la Mnara wa Kumbukumbu ya Mashujaa wa Vita ya Maji Maji mjini Songea.
Kiongozi huyo Mtendaji MKuu wa CCM, amekuwa na ziara ya kikazi ya siku tano mkoani Ruvuma ikiwa ni mwendelezo wa ziara ya siku 10 katika mikoa ya Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Ruvuma.
Lengo la ziara hiyo ya mikoa sita iliyohitimishwa mkoani Ruvuma lilikuwa ni kuimarisha uhai wa chama, kutatua kero za wananchi, kuelezea maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu na Uchaguzi Mkuu mwakani, kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya chama hicho.
Credit: Kusini News

Post a Comment