DC Nyasa awataka Wananchi kushiriki uchaguzi wa Serikali

 

Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mh. Peres Magiri, amewataka wananchi wa Wilaya ya Nyasa kushiriki kikamilifu Uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajia kufanyika mwaka huu 2024.

Ameyasema hayo katika Kijiji ncha Ndengere Kata ya Mbamba bay tarehe 17/04/2024 Wilayani Nyasa, wakati akiongea na wananchi wa Kijiji hicho katika mkutano wa hadhara wenye lengo la kujitambulisha kwa wananchi, kusikiliza kero za wananchi na kutatua.

Mh.Magiri amefafanua kuwa mwaka huu 2024 kutakuwa na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa hivyo wananchi, wanatakiwa kushiriki kwa kujitokeza kugombea na kuchagua kiongozi bora atakayewaletea maendeleo.

Ameongeza kuwa ushiriki wa wananchi ni muhimu sana Katika Uchaguzi kwa kuwa kama tutashirikiana kuchagua viongozi bora, malalamiko yatapungua Ngazi ya Vijiji na Kata na kero zitatatuliwa kwa wakati.

“Ninawaomba wananchi tujitokeze kwa wingi kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uchaguzi utakaofanyika Mwaka huu,ninawataka wanawake pia mshiriki uchaguzi huu kwa kuchukua fomu za kugombea nafasi za Uongozi”

Ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Nyasa ni ya siku 3 na inafanyika katika Kata ya tarehe 17/04/2024 Mbambabay, Kilosa tarehe,18/04/2024, na Mbaha ni tarehe 19.04.2024

Katika Hatua nyingine amewataka wananchi hao kujitokeza kwa wingi kumlaki Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Dkt Emanuely Nchimbi atakayefanya Ziara ya Kikazi Wilayani Nyasa Tarehe 21/04/2024 atakayefanya Mkutano wa Hadhara katika Viwanja Vya Bandari Mjini Mbamba bay.

Credit: www.nyasadc.go.tz

No comments