Baraza la vita la Israel latofautiana kuhusu muda na ukubwa wa jibu la shambulio la Iran

 

Nchini Israeli, shule zilifungwa, na mikusanyiko ya hadhara kuzuiliwa kama tahadhari kabla ya Iran kurusha makombora na ndege zisizo na rubani zaidi ya 300, lakini uamuzi wa kulegeza msimamo uliotangazwa na jeshi la Israel jana usiku unaonyesha tishio la wimbi jipya la mashambulizi limepita.

Kwa upande mwingine, baada ya masaa matatu ya mashauriano, Baraza la Vita la Israel, katika kikao chake cha jana, halikufikia uamuzi wa namna ya kujibu mashambulizi ya Iran.

Baraza la Vita linasemekana kuunga mkono ulazima wa jibu, lakini limegawanywa kulingana na muda na kiwango cha jibu hilo.

Israel inasema kuwa ndege na makombora yote ya mashambulizi yalitenguliwa nje ya anga yake kwa usaidizi wa washirika wake, huku Iran ikisema ilizipa nchi jirani na Marekani notisi ya saa 72 kabla ya kufanya mashambulizi hayo.

bbc

No comments