Ziara Sekretarieti CCM Pwani Tawi kwa Tawi Kata ya Mlanzi
KIBITI - MLANZI
Sekretarieti ya Chama Cha Mapinduzi CCM (M) Pwani Leo Tarehe *04/03/2024* imekutana na wanaccm wa Wilaya ya Kibiti kata ya Mlanzi katika kikao Chake Cha ndani kilichohusu Maandalizi ya Uchaguzi mdogo wa nafasi ya Udiwani katika Kata hiyo.
Akizungumza na Wanaccm hao Katibu wa CCM Mkoa wa Pwani *Ndg. Bernard Ghaty* amewapongeza Kwa kuwa watulivu baada ya kura za maoni kumalizika, huku akiwakumbusha kuwajibika kikamilifu ili kuhakikisha CCM inashinda.
*Ndg. Ghaty* ameendelea kusema kuwa Kila mwanaccm mwenye sifa na vigezo vya kupiga kura ashawishiwe kuipigia kura ccm mara uchaguzi huo utakapofika.
Amehitimisha kwa kuwahimiza Wanaccm hao kutumia vyema majukwaa kwa Kuelezea Utekelezaji wa ILANI pasipo na kigugumizi chochote.
*"Tunayo sababu ya kushinda uchaguzi huu mdogo kwani Kila mahali Serikali ya ccm imetekeleza kwa kishindo ilani ya uchaguzi 2020 - 2025"* amesema Ghaty
Taarifa hii imetolewa na
David Mramba
Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo CCM Mkoa wa Pwani.

Post a Comment