Serikali imejipanga kuboresha changamoto sekta ya utalii

Serikali imejipanga kuboresha utendaji kazi, kuleta mapinduzi katika utoaji huduma na utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya uhifadhi wa Wanyamapori, ikiwemo utatuzi wa migongano baina ya binadamu na Wanyamapori.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) katika Maadhimisho ya Siku ya Wanyamapori Duniani yenye lengo la kuamsha ari na kuongeza uelewa kwa jamii kuhusu uhifadhi na umuhimu wa matumizi endelevu ya rasilimali za Wanyamapori na misitu yaliyofanyika kitaifa katika  Viwanja vya Stendi ya zamani, Wilayani Babati Mkoani Manyara.

Amesema Serikali imeendelea kukabiliana na changamoto mbalimbali za sekta hiyo za ujangili, biashara haramu ya nyara na mazao ya misitu, uvamizi wa maeneo ya hifadhi, shoroba na mtawanyiko wa wanyamapori, kuingiza mifugo katika maeneo ya hifadhi na mabadiliko ya tabia nchi.

No comments