Watalii 482 waliotembelea Lindi waahidi kuitangaza Tanzania
KIASI cha watalii 482 kutoka nchi mbalimbali barani Ulaya
waliotembelea Kisiwa cha Mafia, wilayani Mafia Mkoani Pwani mwishoni mwa wiki,
wameahidi kuitangaza Tanzania huko waendako.
Wakiwa wamepokewa na Mkuu wa Wilaya ya Mafia, Aziza
Mwangosongo, watalii hao baada ya kufika kisiwani hapo, licha ya kufurahia
manzari nzuri ya kisiwa hicho, lakini pia walijivinjari kwa muziki wa kopi
uliopigwa na wao wenyewe, wakinakili muziki wa hayati Bob Marley.
Aisha, wakiwa ufukweni, watalii hao waliogelea na kupunga
upepo, huku wakiangalia pia samaki wa aina mbalimbali wanaopatikana katika Bahari
ya Hindi iliyopo Kisiwani hapo, ambapo waliwasili kwa meli kubwa ya kitalii
duniani inayofahamika kama The World.

Post a Comment