Nigeria: Rais Tinubu apiga marufuku safari za viongozi Aprili
Rais Tinubu, katika barua yake aliyoiandika, aliagiza kuzuiliwa kwa safari zote za nje, lakini akasema kwamba ruhusa inaweza kutolewa kwa safari zinazoonekana kuwa muhimu sana.
Barua hiyo iliongeza kuwa Tinubu alisema ruhusa hiyo itahitaji idhini ya rais ambayo lazima itafutwe wiki mbili kabla ya safari iliyopangwa.
Kulingana na barua hiyo, marufuku hiyo itadumu kwa siku 90 kwa mara ya kwanza na itaanza kutumika Aprili 1, 2024.
Mkuu wa wafanyikazi wa Bw Tinubu alisema hatua hiyo ilichochewa na "wasiwasi wa rais kuhusu kupanda kwa gharama za usafiri".Marufuku hiyo itaanza kutekelezwa tarehe 1 Aprili.
Rais Tinubu na utawala wake wamekuwa wakikosolewa na baadhi ya watu kwa ziara zao za mara kwa mara nje ya nch

Post a Comment