Mkurugenzi Mtendaji Kasulu ashiriki wiki ya maji
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji Kasulu, Vumilia Simbeye ameshiriki kwenye Maadhimisho ya WIKI LA MAJI; hafla iliyofanyika katika Kata ya Musambara kandokando ya Mto maarufu wa Luchugi ambao chanzo chake ni Halmashauri ya Kasulu vijijini ambapo; Mradi wa Shilingi Bil. 35 fedha zilizotolewa na Mhe. Rais Dkt. SAMIA SULUHU HASSAN unatekelezwa katika kukabiliana na changamoto ya uhaba wa maji safi na salama ndani ya mji wa Kasulu, wilayani Kasulu Mkoani Kigoma.
Mradi unaotarajiwa kukamilika ifikapo Oktoba 2025 na mara tu baada ya ukamilikaji wake changamoto ya uhaba wa maji itabakia kuwa historia kwa wananchi waishio Kasulu Mjini na maeneo jirani.
Sambamba na Mradi huo, Serikali pia kupitia Wizara ya Maji imetoa kiasi cha Shilingi Mil. 700 kwa ajili ya kuchukua hatua za haraka kuboresha miundombinu ya maji katika Halmashauri ya Mji wa Kasulu, ikiwa ni kusafisha maji yaliyokuwa yanaambatana na tope ili waweze kuyatumia kwa kipindi ambacho Mradi huo mkubwa wa miji 28 ukiendelea kutekelezwa.
Mgeni Rasmi katika hafla hiyo alikuwa ni Bi. Theresia Mtewele, Katibu Tawala Wilaya Kasulu ambapo kwa pamoja walipata wasaha wa kuzungumza na wananchi waishio ndani ya Kata ambayo Mradi huo mkubwa unatekelezwa kwa kuwapa elimu na maarifa ya kutosha juu ya umuhimu wa utunzaji wa mazingira na vyanzo vya maji kwani; maji ni uhai.
Hafla hiyo imehitimishwa kwa kupanda jumla ya Miti rafiki 1500 kandokando ya Mto Luchugi na maeneo ya jirani. Miti imepandwa na Mgeni Rasmi, viongozi na mamia ya wananchi waliohudhuria na kushiriki hafla hiyo iliyoandaliwa na Wataalamu wa Maji.
# Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
# Mhe. Mohamed Mchengerwa
# Mhe. Juma Aweso
# Mhe. Prof. Joyce Ndalichako
# Mhe. Thobias Andengenye
# Mhe. Isack Mwakisu
# Kasulu yetu, maendeleo yetu
# Kazi inaendelea

Post a Comment