Mwanasiasa wa ngazi ya juu wa Democratic atoa wito wa kufanyika kwa uchaguzi mpya Israel
Kiongozi wa walio wengi katika Bunge la Seneti nchini Marekani Chuck Schumer ametoa wito wa kufanyika kwa uchaguzi mpya nchini Israel, akimshutumu Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kwa kutanguliza "uhai wake wa kisiasa" badala ya maslahi ya nchi hiyo.
Bw Schumer, mwanachama wa chama cha Democratic na afisa wa ngazi ya juu zaidi wa Kiyahudi nchini Marekani, alisema Bw Netanyahu "amepotea mwelekeo".
Alionya kwamba majeruhi makubwa ya raia huko Gaza yanatishia kuleta mvutano baina ya washirika na kuifanya Israel "kutengwa" ya kimataifa.Huu ni ukosoaji mkubwa wa kiongozi wa kisiasa wa Marekani dhidi ya serikali ya Bw Netanyahu.
Maafisa wa Washington, akiwemo Rais Joe Biden, wame]jiepusha ukosoaji wa moja kwa moja wa mtazamo wa Bw Netanyahu katika mzozo huo, ambao ulianza wakati wanamgambo wa Hamas wenye silaha walipovamia kusini mwa Israel tarehe 7 Oktoba, na kuua takriban watu 1,200 na kuwachukua mateka wengine 253.
Hata hivyo, nyufa zimeanza kujitokeza katika muungano huo wiki za hivi karibuni, huku rais akiionya Israel dhidi ya kupanua uvamizi wake katika mji wa Rafah, ambao aliuita "mstari mwekundu".
Hata hivyo, Ikulu ya White House imejitenga na kauli ya Bw Schumer.
Msemaji John Kirby alisema kwamba wakati kiongozi wa Seneti alikuwa na haki ya maoni yake, maafisa wa utawala walilenga kufanya kazi na Israeli katika utetezi wake.
bbc

Post a Comment