MKOA WA DODOMA WAANZA MAANDALIZI YA AFCON YA 2027

 

NA JOHN BANDA, DODOMA

MKUU wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amezitaka Taasisi na Wadau mbalimbali wa Michezo kuanza kujiandaa  Kuweka mazingira mazuri ili kuweza kuyapokea na kuyatendea haki madhindano ya AFCON yatakayofanyika mwaka 2027

Rosemary Ameyasema hayo wakati akizindua Juma la Elimu lililoanza Leo Machi 19,2024 Kwa kuanza michezo mbalimbali  ikishindanisha wanafunzi kutoka shule tofauti za sekondari na Msingi mkoani humo

Mashindano ya AFCON Yamepangwa Kufanyika katika Nchi za Africa Mashariki na Kati Tanzania ikiwemo ambapo Shirikisho la Soka Africa Caf limezitaka Nchi hizo kujiandaa vizuri.

"Inawezekana Mkoa wa Dodoma ukawa ni mmoja wa Miako ya Tanzania itakapofanyokia Michezo ya AFCON itakayofanyika mwaka 2027, hivyo hatuna budi kuanza kujiandaa Mapema Kwa kuweka mazingira wezeshi Kwa michezo hiyo kwa ajili ya wageni", amesema

Aidha Mkuu wa Mkoa  Huyo amewataka Walimu wakuu kusimamia Zoezi la mbio za pole maarufu Mchakamchaka mashuleni kuanzia sasa kwa lengo la kuwafanya kuwa na utimamu wa Kimwili, kiakili pamoja na kuwajengea Uzalendo wanafunzi kutokana na nyimbo zinazotumiwa.

"Asilimia 30 ya magonjwa yanayosumbua watu ni Yale yasiyo ya kuambukiza yanayosababishwa na watu kutofanya mazoezi, niombe tuwasimamie watoto wetu wafanye mazoezi ili tuwaepushe na Garama za matibabu yasiyo ma ulazima huku tukiwajenga katika uzalendo", amesema

Sambamba na Hilo Senyamule amepokea na kugawa mipira 1,000 iliyotolewa na shirikisho la Mpira Wa miguu Tanzania na kuigawa kwa Wilaya zote 7 za mkoa huo kwa lengo la kuendeleza michezo na kuibua vipaji mashuleni.

"Rais Samia apewe Maua yake maana sote tunajua baada ya kuingia madarakani michezo imekua ambapo baadhi ya vilabu vyetu Vimeingia Robo fainali ya Mashindano ya Vilabu Barani Africa CAF na sasa anataka tuendeleze vipaji vya michezo kuanzia kwenye shule zetu, tunamshukuru pia Rais wa Tff Bwana Karia kwa kutupatia mipira hii 1,000 ambayo itasaidia kwa kiwango kikubwa", amesema.


Awali RC Senyamle ameshiriki Mchakamchaka na baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari mkoani humo.

Kwa Upande wake Afisa Elimu wa Mkoa wa Dodoma, Vicent Kayombo amesema Uzinduzi wa Juma la Elimu unaambatana na kuwajengea wanafunzi ukakamavu kupitia Skauti, kufanya mazoezi ya viungo, kukimbia mchakamcha ikiwa ni pamoja na kushiriki michezo mbalimbali

"Uzinduzi huu Wa wiki ya elimu umeambatana na Uzinduzi wa Bonanza la michezo kwa Wanafunzi", amesema

No comments