Kocha wa Tabora United afungashiwa virago
Uongozi wa Klabu ya Tabora United imefikia makubaliano ya pande zote mbili ya kusitisha mkataba na aliyekuwa Kocha Mkuu Goran Copnovic raia wa Serbia kuanzia leo Machi 21.
Tabora United imefikia uamuzi huo kutokana na kutorodhishwa na mwenendo wa matokeo ambayo Timu hiyo imekuwa ikiyapata katika michezo yake ya Ligi Kuu ya NBC Soka Tanzania .
Goran Copnovic alijiunga na Tabora United Agosti mwaka jana kama kocha mkuu kwa mkataba wa mwaka mmoja ambao ulikuwa umalizike mwishoni mwa msimu huu kabla ya kufikia uamuzi wa kuvunjwa mapema leo hii.
Tabora United inamshukuru Kocha Goran kwa utumishi wake tangu alipojiunga na Timu na hivyo inamtakia kila la heri huko aendako.
Imetolewa leo Machi 21, 2024
Na Christina Mwagala
Mkuu wa Idara ya Habari na na Tabora united.

Post a Comment