Forums General Forums International Forum Rais wa Senegal akubali kubadili tarehe ya Uchaguzi Mkuu baada ya shinikizo la Maandamano

 


SENEGAL: Rais Macky Sall amekubali kufanya mabadiliko ya tarehe ya Uchaguzi Mkuu kutoka Desemba 15, 2024 hadi Machi 24 kutokana na maandamano yanayomtaka kuheshimu muda wake wa kuondoka madarakani.

Awali Rais Sall anayetakiwa kumaliza kupindi cha utawala wake kwa mujibu wa Katiba ifikapo Aprili 2, 2024 alipeleka Muswada Bungeni na uliosogeza mbele Uchaguzi na kumpa kibali cha kubaki madarakani hadi Desemba 2024 hali iliyozua vurugu nchini humo.

Taarifa kutoka Senegal zimekuwa zikiripoti kuwa awamu ya pili ya Rais Sall ilitawaliwa na Ukandamizaji wa Wapinzani wake ambapo takriban Watu 1,000 walifungwa jela kwa kumpinga hadharani Kiongozi huyo.

Aidha hivi karibuni Bunge la nchi hiyo lililazimika kupitisha Sheria ya kutoa msamaha kwa Wafungwa wa Kisiasa ili kuepusha Taifa hilo kuingia katika machafuko zaidi.


No comments