DC Mbinga aunga mkono maendeleo shule ya wazazi Mkinga Sekondari


Chama Cha mapinduzi wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma, kupitia jumuiya ya wazazi- CCM Leo Mach 27- 2024  Kimepokea mchango kutoka Kwa Mkuu wa wilaya ya Mbinga Mhe. Kisare Makoli kiasi Cha Fedha Shilingi laki Tano (500,000) ikiwa ni mchango kwaajili ya ukarabati wa madarasa ya kidato Cha Tano na sita katika shule ya Mkinga Sekondari inayomilikiwa na CCM na kusimamiwa na Jumuiya ya wazazi Tanzania.


Wakishukuru katika Hafla hiyo fupi iliyofanyika ofisi ya mkuu wa wilaya ya mbinga, Mwenyekiti wa Bodi ya shule hiyo Ndugu Daniel Chindengwike pamoja na katibu wa jumuiya ya wazazi CCM wilaya ya Mbinga comrade Angelo Madundo wamemshukuru DC Kwa Mchango huo uliotolewa na ofisi yake kwa ajili ya Maendeleo ya shule ya wazazi Mkinga iliyopo Km. 10 kutoka Makao makuu ya Halmashauri ya Mbinga Mji.

Imetolewa na Ofisi ya Jumuiya ya wazazi CCM wilaya ya Mbinga 27/03/2024.


No comments