DC IRINGA KHERI JAMES:TUSIWANYIME VIJANA UHURU WA KUTOA MAONI

 


MKUU  wa Wilaya ya Iringa Kheri James akiwasilisha mada kwenye mdahalo huo inayohusu"Mchango wa wasomi katika siasa na maendeleo ya Taifa, alisema vijana wasomi wanalojukumu la kuwa na Uhuru wa kutoa maoni ili wanapokosea na kukoselewa waweze kujifunza. 

Ameyasema hayo wakati akiwasilisha mada inayosema"Mchango wa wasomi katika siasa na maendeleo ya taifa"kwenye mdahalo  wa siku mbili wa Seneti ya vyuo na vyuo vikuu,ulioanza kufanyika  Jana  katika ukumbi wa chuo Cha ufundi Ihemi kinachomilikiwa na UVCCM,kilichopo wilayani Iringa Mkoani humo.

Alisema kukosea ndio mwanzo wa kujifunza, hivyo vijana wakikosea isiwe change cha kuwatengenezea usaliti. 

"Inashangaza kuona vijana wakikosea, matokeo yake wanaambiwa mpinzani, kwakufanya hivyo kunapelekea vijana kuingiwa na uwoga  wa kuongea na kutoa maoni yao"Alisisitiza.

No comments