Ziara ya Mwenyekiti CCM Pwani yatikisa Kibaha Vijijini


Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani *Ndg. Mwinshehe Shaban Mlao (MNEC)* amefanya ziara ya Siku moja katika Wilaya ya Kibaha Vijijini akiongozana na Kamati ya Siasa ya  alitembelea na kukagua ujenzi wa Soka kuu la Mlandizi ambapo amepongeza jitihada zinazoendelea katika Ujenzi huo, Pia ametembelea kujionea uwekezaji wa Viwanda katika eneo la KAMAKA ambapo ameipongeza Serikali ya wamau ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania *Mhe Dkt Samia Suluh Hassan* kwa kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji wa Nje na ndani ya Nchi

Vilevile amefanya kikao cha ndani ambapo alikutana na Wajumbe wa Halmashauri kuu ya Wilaya na Mabaraza ya Jumuiya za Chama, amabapo amewataka Viongozi wote kujipanga vyema kushiriki uchaguzi kwa Uadirifu na kuhakikisha CCM Inashinda kwa Kishindo

Mwisho, Mwenyekiti Mlao alihitimisha kwa kuongea na Wanachama pamoja na Wananchi katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mtongani ambapo amepokea kero za Wananchi na kujibiwa na Watendaji wa Serikali, pamoja na hayo alikabidhi Kadi za BIMA ya Afya 106 kwa Wananchi wa Kata ya Mtambani ambazo zimetolewa na Mheshimwa Diwani wa Kata ya Mtambani *Mhe Godfrey Mwafulilwa* vilevile Mbunge wa Jimbo la Kibaha *Mhe Michael Mwakamo* alilezea Mambo yote aliyosimamia na kutekelezwa na Serikali ya CCM akishirikiana na Madiwani wa Halmashauri ya Kibaha kwa kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania *Mhe Dkt Samia Suluh Hassan*




Imetolewa na

Idara ya Siasa na Uenezi, Wilaya ya Kibaha Vijijini

No comments