Waziri Mkuu shoga wa Ufaransa amteua mumewe kuwa Waziri wa Nje

Waziri Mkuu mpya wa Ufaransa Gabriel Attal ambaye ni shoga amemteua mume wake Stephane Sejourne kuwa waziri wa mambo ya nje, siku chache tu baada ya yeye kuwa shoga wa kwanza aliyejinadi hadharani kushikilia wadhifa wa uwaziri mkuu wa nchi hiyo.

Sejourne, ambaye pia anaongoza chama cha siasa cha Rais Emmanuel Macron cha Renaissance na kundi la Renew katika Bunge la Ulaya, anachukua nafasi ya Catherine Colonna katika mabadiliko ya baraza la mawaziri yaliyofuatia kujiuzulu kwa waziri mkuu wa zamani Elisabeth Borne siku ya Jumatatu.

Waziri huyo mpya wa mambo ya nje mwenye umri wa miaka 38 alikuwa mshauri wa Macron tangu akiwa Waziri wa Uchumi na Fedha, kisha akajiunga na timu yake mwaka 2014 na kubaki naye katika katika kampeni za uchaguzi wa Rais mwaka 2017.



No comments