WATUHUMIWA 13 WAKAMATWA KWA KUCHOMA MOTO BASI LA SAI BABA KOROGWE

 

Jeshi la Polisi Mkoani Tanga limesema mpaka sasa wamefanikiwa kuwakamata Jumla ya Watuhumiwa Kumi na Tatu (13) kuhusiana na Tukio la Kuchoma gari namba T.668 BCD Scania Mali ya Kampuni ya Sai Baba, katika Kata ya Msambiazi, Tarafa ya Korogwe, wilaya ya Korogwe.

Hayo yamebainishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, ACP Alimachius Mchunguzi wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ofisi yake Jijini Tanga ambapo amesema Mara baaa ya Upelelezi kukamilika watuhumiwa hao watafikishwa Mahakamani

Amesema katika Tukio hilo, Basi la SAI BABA  likiendeshwa na Seasa Frank Chuwa (48) Mkazi wa Dar es Salaam likitokea katika Mkoa huo kuelekea mkoa wa Arusha liligongana na Pikipiki namba MC 819 EAF aina ya Hajoue iliyokuwa ikiendeshwa na Awadh Issa Juma (20) Mkazi wa Mtonga Korogwe akitokea Msambiazi kuelekea Korogwe na kusababisha kifo kwa dereva huyo wa Pikipiki na Uharibifu wa Gari.

Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga limetoa wito kwa Baadhi ya Wananchi ambao bado wanaendelea kujihusisha na vitendo vya kihalifu kuacha kwani wakiendelea Jeshi halitosita  kuwakamata na kuwafikisha Mahakamani. 


No comments