Pogba afungiwa kucheza soka miaka minne kwa matumizi dawa zilizopigwa marufuku

 

Kiungo wa Juventus Paul Pogba amefungiwa kucheza mpira kwa miaka minne kutokana na kosa la kutumia dawa zilizopigwa marufuku.
Alifungiwa kimsingi mwezi Septemba mwaka jana baada ya vipimo vya awali kuonesha viwango vikubwa vya testosterone mwilini mwake.
Pogba, 30, alifanyiwa vipimo vya ghafla baada ya mechi ya kwanza ya Juventus ya msimu, Agosti 20.
Alipewa hukumu hiyo na mamlaka ya kupambana na dawa michezoni ya Italia (Nado).
Vipimo vya pili vilithibitishwa na Nado katika sampuli ya pili mwezi Oktoba, na ofisi ya mwendesha mashaka wa Nado ilipendekeza adhabu ya kufungiwa miaka minne.
Hukumu hii inamaaanisha Pogba hatoweza kucheza hadi mwaka 2027, ambapo atakuwa na umri wa miaka 33. Adhabu ilisogezwa nyuma kuanzia pale alipopimwa kwa mara ya kwanza.
Taarifa zinasema Pogba anaamini hakunywa dawa hizo kwa makusidi ila kwa kutokufahamu.

Testosterone ni homoni ambayo inaongeza uthabiti kwa wanamichezo.

No comments