Watanzania waishio nje ya nchi wanaleta nyumbani fedha kiduchu kuliko Wakenya
Somalia, ambayo muda mwingi iko vitani wenyewe kwa wenyewe, wananchi wake wanaleta nyumbani kiasi cha shilingi trilioni 4, huku Congo DR, ambayo na yenyewe muda mwingi iko vitani, inapokea shilingi trilioni 3.2.
Uganda yenyewe inapokea shilingi trilioni 3 kutoka kwa raia wake wa nje, wakati Sudan ya Kusini yenyewe wananchi wake walio nje huwaletea kiasi cha shilingi trilioni 2.7 na Rwanda, moja ya nchi zinazotajwa uchumi wake kupaa kwa kasi, hupokea kiasi cha trilioni 1.3.

Post a Comment