DC Mbinga akagua nyumba ya Mkurugenzi, azungumza na wazazi wanafunzi shule ya Kitumbalomo
Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mhe.Aziza Ally Mangosongo akiambatana na wajumbe wa kamati ya usalama Wilaya, alifanya ziara ya kukagua ujenzi wa nyumba ya Mkurugenzi na Nyumba za wakuu wa idara wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga pamoja na kutembelea na kuzungumza na wazazi na wanafunzi wa shule ya sekondari ya kata ya kitumbalomo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyowasilishwa na afisa mipango Ndugu Christopher Ntandu kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Juma Haji Juma Alibainisha kwamba nyumba ya Mkurugenzi imegharimu kiasi cha zaidi ya Tshs 333M, ikiwa milioni 33 fedha za mapato ya ndani na 300M kutoka serikali kuu.
Vilevile, Nyumba za wakuu wa idara ujenzi unaendelea na zitagharimu kiasi cha Tshs 360M, Ikiwa 240M kutoka serikali kuu na 120M ni mapato ya ndani, Aidha ujenzi wa shule mpya ya kisasa wa sekondari ya kata ya kitumbalomo umegharimu jumla ya zaidi ya Tshs 742M, ikiwa serikali kuu ilitoa 560M na 182M ni fedha za mapato ya ndani kujenga majengo tisa ambayo yamekamilika na tayari masomo yameanza kwa wanafunzi 153.
Aidha, Mkuu wa Wilaya Mbinga alimshukuru Mhe.Rais, Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha hizo kwa lengo la kuboresha mazingira ya watumishi na kuondoa adha ya wanafunzi kutembea umbali mrefu zaidi ya km15 kufuata huduma za elimu kata jirani ya matiri, Hivyo basi nitoe rai kwenu wazazi na walimu kuhakikisha watoto wanahudhuria masomo na kudhibiti utoro ili ujenzi wa shule hiyo uwe na tija na kuleta manufaa makubwa.
Hata hivyo, Aliitaka halmashauri dosari na kasoro zote zilizoainisha wakati wa ukaguzi zifanyiwe marekebisho kwa wakati, kuzingatia ukomo wa muda wa miradi, Vilevile aliwataka mafundi kuwa waaminifu, kutekeleza miradi yenye ubora pamoja na kuacha tabia ya wizi wa vifaa hali ambayo uchelewesha miradi.
Sambamba na hilo alitoa wito kwa wazazi kuchangia chakula shuleni, Vilevile kufuatilia maendeleo ya kitabia na kitaaluma ili waweze kutimiza ndoto zao, Ikiwa pamoja kudhibiti utoro na kutoa elimu ya malezi ili kuepusha mimba, Aidha, Aliwataka walimu,wanafunzi na wazazi kuhakikisha miundombinu inatunzwa.
Vilevile, Alitoa wito kwa wananchi kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka ilj kuchagua viongozi watakosukuma maendeleo mbele, Vilevile alisisitiza kutimiza afua za lishe na kuhakikisha wanafunzi wanapata mlo kamili ili kuwaepusha na athari za udumavu.
Mwisho, Nae Diwani wa kata ya kitumbalomo Denis Kapinga, alimshukuru Mhe. Rais, Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kupata mradi huo kwasababu umehitimisha changamoto ya muda mrefu ya wananfunzi kutembea zaidi ya km15 kufuata huduma za elimu, Sambamba na hilo alimshukuru kwa kutekelezewa kwa miradi mingine ikiwemo maji, umeme na afya.
Imetolewa na
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Mbinga
February 12, 2024

Post a Comment