Wasanii marafiki, Msechu na Mpoto kumuaga Lowassa kwa nyimbo, tenzi

Wasanii marafiki wa Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa, Peter Msechu na Mrisho Mpoto wataimba nyimbo na tenzi wakati wa mazishi ya kiongozi huyo yatakayofanyika leo huko Monduli.

Kwa mujibu wa Ratiba iliyotolewa na Kamati ya Mazishi Kitaifa, inayoongozwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, wasanii hao ni miongoni mwa watu wa makundi mbalimbali waliopewa nafasi ya kutoa salamu za pole wakati ya mazishi hayo yanayosimamiwa na serikali.

Licha ya wasanii hao, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela na Spika wa Bunge, Tulia Aktson nao pia watatoa salamu za pole na baadae, mtoto wa marehemu, Fredrick Lowassa atatoa salamu za familia.

Kisha, Mwenyekiti wa Kamati ya mazishi kitaifa, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa atatoa salamu kabla ya kumkaribisha Rais Samia kutoa salamu zake za pole kwa niaba ya Watanzania.


No comments