RC Makongoro akagua miradi Sumbawanga, apongeza, ataka juhudi zaidi

Mheshimiwa Charles Makongoro Nyerere Mkuu wa Mkoa wa Rukwa amefanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga tarehe 16 Februari 2024.

Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa amekagua maendeleo ya ujenzi wa shule mpya ya Sekondari ya Kata ya Kalumbaleza, ujenzi wa wodi na Jengo la Huduma za Dharura katika Hospitali  ya Wilaya ya Sumbawanga na ujenzi wa shule mpya ya Msingi Lanchi iliyoko Mtowisa.

Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kwa kukamilisha ujenzi wa shule mpya ya Lanchi na kuwezesha kuanza kwa masomo.

Ameitaka Halmashauri ya Sumbawanga kukamilisha kwa wakati ujenzi wa shule mpya ya Sekondari ya Kalumbaleza ili kutatua kero ya wanafunzi kutembea umbali mrefu.

Mheshimiwa Makongoro ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kukamilisha ujenzi wa wodi zote na Jengo la Huduma za Dharura ili  wananchi wapate huduma zote katika hospitali ya Wilaya kama ilivyokusudiwa na Serikali.


No comments