Viongozi mbalimbali watoa neno kuagwa kwa Lowassa

 

Jaji Joseph Warioba

1995 Lowassa alinitafuta akiwa na uchungu sana baada ya kuambiwa Nyerere ndio aliyetia ugumu kuwania Urais. Nilimtia moyo, hakukata tamaa.

2008 Lowassa alinitafuta baada ya kujiuzulu, alisema hakutendewa haki, wamemuhukumu bila kumsikiliza, alinitafuta tukazungumza, nilimwambia haya ni mambo ya kisiasa, asikate tamaa.

Alikuwa alipenda elimu, ni mtu mwenye imani kuwa ana wajibu wa kutumikia taifa, hakuwa mangimeza, alikuwa mtu wa vitendo, pamoja na mapungufu yake hakuwa mtu anayependa kugombana na watu, alikuwa kiongozi mvumilivu, alikuwa ni kiongozi mwenye sifa ya kuwa kiongozi, mwenye maono.

No comments