Urusi yadaiwa kuwaua wanajeshi wa Ukraine hata baada ya kusalimu amri Avdiivka
Wiki iliyopita, vikosi vya Ukraine vilisalimisha mji wa mashariki wa Avdiivka, ambao kwa muda wa miezi kadhaa wamekuwa wakiulinda kwa nguvu dhidi ya uvamizi wa kikatili wa Urusi.
Ushindi wa Avdiivka unawakilisha ushindi wa kimkakati na wa kiishara kwa Urusi, kuimarisha ulinzi wake wa mji mkuu wa mkoa, Donetsk, na uwezekano wa kufungua njia za mashambulio zaidi dhidi ya eneo linaloshikiliwa na Ukraine.
Kamanda mkuu wa Ukraine Oleksandr Syrskyi anasema aliamuru kutoroka kutoka mji huo ili kuokoa maisha ya wanajeshi.
Sasa ushahidi wa uwezekano wa uhalifu wa kivita umeibuka, huku jamaa za wanajeshi sita waliopatikana wamekufa kufuatia kutwaliwa kwa jiji hilo wanasema waliuawa baada ya kujisalimisha. Mamlaka ya Ukraine inachunguza. Moscow bado haijatoa maoni.
BBC imezungumza na wanajeshi wa Ukraine waliojiondoa kutoka Avdiivka. Ushuhuda wao unatoa taswira ya makamanda wasioitikia waliokataa ombi la askari wao la kutaka kurudi nyuma walipokuwa wamezingirwa na wanajeshi wa Urusi.

Post a Comment