Ujenzi shule ya Mkoa Katavi wafikia asilimia 80
NAIBU Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Deogratius Ndejembi amesema ujenzi wa Shule ya Sayansi ya Wasichana Mkoa wa Katavi imefikia asilimia 80 ili iweze kukamilika.
Mhe Ndejembi amesema hayo leo bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Katavi, Mhe Martha Mariki aliyetaka kujua ni lini serikali itatekeleza ahadi ya ujenzi wa shule hiyo.
“ Ujenzi wa Shule ya Bweni ya Wasichana kwa ajili ya masomo ya Sayansi katika Mkoa wa Katavi unafanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Kata ya Katalala ambapo hadi sasa ujenzi upo asilimua 80. Shule hii imesajiliwa na kuandikisha Wanafunzi 100 wa kidato cha kwanza mwaka 2024,” Amesema Mhe Ndejembi.

Post a Comment