Mh Mbunge Festo Sanga alia na riba kubwa za mabenki kwa watumishi


Mbunge wa Jimbo la Makete Mhe. Festo Sanga amepaza sauti Bungeni leo tarehe 14/02/2024 akichangia hoja ya Kamati ya Bajeti ambapo kilio chake kwa Serikali ni namna mabenki Nchini yanavyoumiza watumishi kwenye riba za mikopo.

Mhe. Sanga amesema " Uhai wa Benki zetu Nchini zinabebwa na Watumishi, lakini kiwango cha riba wanachotozwa wanapokopa ni kikubwa sanaa kinyume na uhalisia, riba hizo zimegeuka mwiba mchungu kwa watumishi wetu wazalendo hapa Nchini, Benki hizi zinapata riba ndogo wanapokopa Benki Kuu, lakini wao wanatoza riba kwa watumishi bila kujali mchango wao kwenye uhai wa hizo Benki,"

Anaendelea kusema "Benki nyingi zinapata faida kwa Horizontal gain hawahangaiki kwenda kutafuta wateja wengine ambao wangesaidia kuongeza mzunguko wa fedha kwenye mabenki na kuwapunguzia mzigo watumishi, kila jicho la benki linaangalia namna ya kupata faida kwa mtumishi aidha kwa makato au kwa riba kwenye mikopo, kwanini hawajawekeza kwenye Rural Banking?, Watanzania wengi wanafedha huko vijijini lakini hawana elimu ya Benki".

Mwisho ameshauri kwa kuongeza kuwa "Gavana kupitia Benki kuu kupitia upya mchakato wa mabenki yanavyopanga riba, vilevile Waziri wa Fedha aunde kikosi kazi kufuatilia Microfinance zinazotoza riba kinyume na utaratibu".

No comments