Sanamu ya Baba wa Taifa Makao Makuu AU yaleta sintofahamu

Rais Samia Suluhu Hassan leo alishiriki uzinduzi wa Sanamu ya Baba wa Taifa pale Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) Addis Ababa nchini Ethiopia.

AU imeweka sanamu hiyo kwa kuthamini mchango wa muasisi huyo wa nchi yetu katika kupigania ukombozi na uhuru wa nchi za bara la Afrika.

Hata hivyo, kwa mujibu wa maoni ya watanzania katika mitandao mbalimbali  ya kijamii, wameonyesha kutokubaliana na sanamu hiyo, wakitoa sababu kadhaa.

Mojawapo ni kutofanana kwa sura kati ya sanamu hiyo na Baba wa Taifa, lakini pia wakikosoa vazi, linaloonekana kumpyaya, tofauti na uvaaji wa enzi za uhai wake.

No comments