RC MAKONGORO AWATAKA WAZAZI KUKAMILISHA RATIBA ZA CHANJO KWA WATOTO MKOANI RUKWA

 


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mheshimiwa Charles Makongoro Nyerere amewataka wazazi Mkoani Rukwa kuhakikisha wanawapeleka watoto wao kupata chanjo kila zinapotangazwa na Serikali na kuhakisha watoto wanakamilisha ratiba za chanjo husika sawa na maelekezo ya wataalam. Amesema kwa kufanya hivyo magonjwa ya milipuko yatadhibitiwa.

Mheshimiwa Makongoro ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa kikao cha Kamati ya Afya ya Msingi ngazi ya Mkoa kilichofanyika Februari 14, 2023 kutathmini maandalizi ya kampeni ya kitaifa ya chanjo ya Surua na Rubella.

Pamoja na maandalizi ya chanjo hiyo itakayotolewa kwa siku tatu kuanzia tarehe 15 hadi 18 Februari 2024, kikao kilipitia na kutathmini hali ya udhibiti wa magonjwa ya mlipuko na tathmini ya utekelezaji wa mkataba wa lishe.

Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa amewataka watoa huduma kuhakikisha wanashirikiana na jamii katika kampeni hiyo ili kuwafikia watoto wote wenye umri wa miezi 9 hadi 59 ili kuikamilisha kampeni hiyo kwa ufanisi.

Mkoa wa Rukwa umelenga kutoa chanjo ya Surua na Rubella kwa watoto 196,961, chanjo hiyo itatolewa katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya na maeneo yote yenye mikusanyiko wa watu.

No comments