Mchezo wa Simba dhidi ya Mtibwa waahirishwa

 


BODI ya Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara, imeusogeza mbele mchezo wa Ligi Kuu kati ya Simba na Mtibwa, uliokuwa uchezwe Jumapili hii katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, ili kutoa nafasi kwa klabu hiyo ya Dar es Salaam kufanya maandalizi ya mchezo wake wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Asec Mimosas ya Ivory Coast.

Katika taaarifa iliyotolewa leo na Idara ya Habari na Mawassiliano ya Bodi ya Ligi, imesema Simba itacheza na Asec Ijumaa ya Februari 23 mwaka huu, hivyo mchezo wake wa ligi dhidi ya Mtibwa utapigwa siku itakayopangwa baadaye.

No comments