Kampuni 3 za China zapendekezwa kujenga Barabara ya Njia 4 ya kulipia Tozo (Kibaha-Mlandizi-Chalinze)
Serikali ya Tanzania kupitia Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) imefanya mchujo wa kampuni 9 na kubakiza 3 ambazo zitashindanishwa kwaajili ya kupata 1 itakayojenga Barabara ya Njia 4 kutoka Kibaha-Mlandizi-Chalize).
Mradi huo utakaogharimu takriban Tsh. 858,500,000,000, utahusisha ujenzi wa Barabara yenye urefu wa Kilomita 78.9 kwa ufadhili Sketa Binafsi na Umma ambayo itakuwa na malipo ya Tozo kwa Watumiaji wake.
Kampuni zilizoorodheshwa ni China Communications Construction Company Ltd (CCCC), China Railway Construction Corporation Ltd (CRCC) na muungano wa China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) na China Railway Construction Engineering Group (CRCEG).
Kwa mujibu wa taarifa, Ujenzi wa Barabarab ya Kibaha-Mlandizi-Chalinze utafuatiwa na ujenzi mwingine wa Kilomita 126.1 kutoka Chalinze hadi Morogoro na Kilomita 258 kutoka Morogoro-Dodoma.

Post a Comment