JUMUIYA YA WAZAZI CCM WILAYA YA MBINGA YASISITIZA MSINGI WA MALEZI NA MAADILI MEMA KWA WATOTO
Katibu wa jumuiya ya wazazi CCM wilaya ya mbinga Mkoani Ruvuma comrade Angelo Madundo Leo Feb 28-2024 ukumbi wa Oddo Mwisho Amekutana na kamati Ndogo ya Elimu malezi na utafiti ya jumuiya hiyo wilaya pamoja na waratibu wa Elimu Kata, kutoka Kata zote 19 za halmashauri ya Mbinga mji kwaajili ya kujengeana uwezo hususani mkakati wa pamoja katika kijiimarisha vyema kwenye ajenda ya Elimu, Malezi na MAADILI mema Kwa wanafunzi Mashuleni.
Comrade Madundo amewataja maafisa/ waratibu wa Elimu Kata ndio kiungo kikubwa Cha kuchochea Kwa haraka maendeleo ya Elimu ngazi ya kata pamoja na kuwa walezi mhimu kati ya Mzazi, Mwalimu na Mwanafunzi, hivyo ofisi ya wazazi CCM wilaya itaendelea kutoa ushirikiano wa kutosha Ili kuhakikisha serikali ya wilaya ya mbinga na chama Cha mapinduzi CCM wanafanikiwa kufikia Malengo ya maboresho hasa huduma ya Elimu inayoendelea kutolewa kwenye nyanja ya msingi na sekondari ndani ya wilaya na halmashauri nzima ya Mbinga mji.
Nae Mwenyekiti wa kamati ya elimu, malezi na utafiti ya jumuiya ya wazazi wilaya Mwalimu Messiah Nyagawa amemshukuru katibu Madundo Kwa kupata Wasaa wa kukutana na waratibu wa Elimu Kata kutoka halmashauri ya Mbinga Mji ili kuwekeana mkakati wa pamoja katika kuhamasisha Umuhimu wa jumuiya hiyo Kwa jamii, pamoja na kutoa semina fupi ihusuyo Elimu ya malezi na maadili Mema.
imetolewa na
Idala ya Elimu, malezi na Mazingira wilaya ya Mbinga*
28/02/2024

Post a Comment