DC MBINGA AZINDUA JENGO KIJIJI CHA ILELA, OFISI ILELA AMCOS NA GARI LAO
Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mhe.Aziza Ally Mangosongo alizindua jengo la Ofisi ya kijiji cha ilela, Ofisi ya Chama msingi cha ushirika (ILELA AMCOS), Sambamba na kuzindua mapokezi ya gari ya mizigo aina ya fuso ambayo imenunuliwa na wanachama. Hafla maalamu ya uzinduzi wa miradi hiyo ilifanyika katika viunga vya ofisi ya kijiji cha ilela.
Akielezea mchakato wa ujenzi wa ofisi, Afisa mtendaji wa kijiji cha ilela Jofrey Ngaponda, Alisema kwamba jengo hilo limegharimu kiasi cha zaidi tshs 38M, Fedha zinazotokana na kodi wa vyumba vya biashara vinavyomilikiwa na kijiji cha ilela vilivyopo Mbinga Mjini.
Ambapo kupitia mkutano wa Kijiji wa 2020 kwa pamoja wananchi waliridhia fedha hizo zitumike kujenga ofisi mpya ya kisasa na ujenzi ulianza mara moja na kukamilika 2022.
Aidha, Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Meneja wa AMCOS ya Ilela Ndugu Gabriel Mapunda, alisema kwamba ofisi ya AMCOS ilela imegharimu kiasi cha Tshs 40M na Gari limenunuliwa kwa gharama ya tshs 96M,
Fedha hizo zimetokana na ushuru wa mazao, Malengo makubwa ni kuokoa gharama za kukodi ofisi na usafiri, Ambapo wanachama kwa pamoja waliibua miradi hiyo mwaka 2024.
Akizungumza na wananchi baada ya kuzindua miradi hiyo Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mhe. Mangosongo alisema "Nimeridhishwa na ubora na thamani halisi ya fedha zilizotumika kutekeleza miradi hii, Niwapongeze viongozi na wananchi kwa wazo na kulitekeleza vizuri"
Vilevile nitoe pongezi wa wanachama wa ilela AMCOS kwa kuibua miradi mikubwa yenye tija ambayo itaokoa gharama za uendeshaji, Kwa kuwa na ofisi na gari ya uhakika muda wote.
Hata hivyo, Mhe. Mangosongo alitoa wito kwa AMCOS na vijiji vingine kuiga mfano huu kwa lengo la kuchochea maendeleo na kuboresha mazingira ya watumishi, Hivyo basi alimtaka afisa ushirika kuzishawishi AMCOS zingine.
Alikadhalika, Alitoa wito miundombinu hiyo itunzwe ili iweze kuwa na tija, Pia aliwataka wanachama na wakulima kuacha tabia ya kutolipa na kulimbikiza madeni hali ambayo uathiri namna bora ya uendeshaji AMCOS.
Aidha, alitumia nafasi hiyo kuwataka wazazi, walimu na wanafunzi kuchukua tahadhari kipindi hiki cha mvua kutojificha maeneo hatarishi, Kutekeleza afua za lishe ili kuepuka udumavu, kupanda miti maeneo ya taasisi, kuacha tabia ya kuwaambia wanafunzi kufeli mitihani kusudi pamoja na kuchangia chakula shuleni ili wanafunzi wafikirie zaidi masomo.
Mwisho, Nae Diwani wa kata ya Mikalanga Mhe. Leonce Nombo alimshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kukabali ombi la kujumuika na wananchi wa ilela kuzindua miradi hiyo, Hali hiyo itaongeza thamani na ufanisi wa kuibua mambo mapya ili kuchochea maendeleo ya kiuzalisha na utoaji huduma kwa wananchi.
Imetolewa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Mbinga
Februari 28, 2024

Post a Comment