Jukwaa La Wazalendo Huru kuikatia Rufaa Sanamu ya Mwalimu Nyerere AU
Jukwaa la Wazalendo Huru Tanzania, linakusudia kumwandikia barua Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, kumuomba Sanamu ya Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere iliyozinduliwa jana katika Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) jijini Addid Ababa Ethiopia ifanyiwe marekebisho, kwani sura iliyopo haiakisi sura halisi ya muasisi huyo wa Taifa la Tanzania.
Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa hilo, Dokta Mohamed Mwampogwa alisema:
"Wazalendo huru tumeangalia Picha ya Sanamu hilo na kujiridhisha kuwa sura hiyo siyo ya Mwl. Julius K.Nyerere. Sanamu ambazo zinafanana kabisa na sura ya Mwl. Nyerere ni kama ile ya Tanga Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, kule Dodoma Nyerere Square hivyo tunayafanya haya kwa nia njema kwa nia ya kuweka Uhalisia katika kumuenzi Mwl.Julius K.Nyerere.

Post a Comment